Mwanafunzi wa chuo ajiua kwa kujinyonga

HomeKitaifa

Mwanafunzi wa chuo ajiua kwa kujinyonga

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) , Gunze Luhangija amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni msongo wa mawazo uliosababishwa na kuvunjika kwa mahusiano yake na mpenzi wake.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limethibitisha tukio hilo na kusema uchunguzi unaendelea.

Baadhi ya wanafunzi chuoni hapo walisema huenda mapenzi yamechangia kwani marehemu alikuwa na ugomvi na mpenzi wake.

“Huyu kijana hapa chuo katusononesha sana wana Mwanza. Siku ya Boxing Day alimnunulia demu (mpenzi) wake iPhone 14 (simu) na baada ya siku chache demu akamkataa kwamba kapata mtu mwingine…dogo kajitundika,” zilieleza taarifa hizo.

Mmoja wa wanafamilia ya marehemu alisema kabla ya kujinyonga, ndugu yao alishakunywa dawa ili kujiua hapo Januari 4 lakini aliokolewa.

Taarifa walizozipata ni kwamba, alisema marehemu alikuwa na mpenzi aliyemgharamia, ikiwamo kumpangishia nyumba.

“Lakini huyu dada alimkataza marehemu asiende kwake kwa madai kuwa anaishi na mdogo wake, ila akapata taarifa kuna vijana wanaenda nyumbani kwa mwanamke huyo, hii ilimpa shida na wakatofautiana , hali iliyompa msongo wa mawazo hata kufanya uamuzi aliochukua,” alisema.

 

error: Content is protected !!