Mabasi 4 ya mwendokasi yatengwa kwa ajili ya wanafunzi

HomeKitaifa

Mabasi 4 ya mwendokasi yatengwa kwa ajili ya wanafunzi

Wakala wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) imetenga mabasi manne makubwa asubuhi na jioni kwa ajili ya kubeba wanafunzi wa shule za msingi na secondary katika njia ya Mbezi – Kimara – Gerezani na Kivukoni.

Mabasi yatabeba wanafunzi kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:20 asubuhi , Mabasi mawili yatapeleka wanafunzi kwa njia ya Kimara hadi Kivukoni na mengine mawili kwenda Gerezani na jioni kuanzia saa 10:30 jioni hadi 11:00 jioni, wanafunzi watatakiwa kupanda mabasi hayo katika vituo vikubwa.

error: Content is protected !!