Rais Samia aeleza maana ya kauli yake ya aliyesimama hapa ni Rais mwenye maumbile ya kike

HomeKitaifa

Rais Samia aeleza maana ya kauli yake ya aliyesimama hapa ni Rais mwenye maumbile ya kike

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kauli yake aliyosema siku ya kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa awamu ya tano, Hayati Magufuli jijini Dodoma ilikua ni ya kuwahakikishia Watanzania kwamba nchi ipo mikono salama na kazi itaendelea.

Amefafanua hayo kwenye hafla ya Kongamano la “The Citizen Rising Women” ikiwa pia ni siku ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.

“Kilichonisukuma kusema tayari kulikua kuna minongono minongono ataweza kweli? kweli inawezekana? mwanamke kweli? lakini nikawaambia aliyesimama hapa ni Rais lakini maumbile yake ya kike. Sasa Rais haina jinsia rais ni rais tu.” amesema Rais Samia.

Rais Samia alisema kauli ili akijua kwamba wananchi wanahofu kwa kuwa kuondokewa na rais akiwa madarakani ni jambo geni kwa Tanzania na pia kuwa na rais mwanamke ni jambo jipya.

Kauli hiyo aliyoisema Rais Samia Machi 22,2021 “ili Kwa wale ambao wana mashaka kwamba Mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwaambie aliyesimama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye maumbile yake ni Mwanamke.”Aidha Rais Samia ameongeza kwa kusema ule ulikua mtihani wake wa kwanza kwani alijua watu wengi walikuwa wakijiuliza atawezaje.

Miaka mitatu ya uongozi 

Tarehe 19 mwezi huu, Rais Samia anatimiza miaka mitatu akiwa madarakani na watanzania wameshuhudia kazi kubwa aliyoifanya kwenye kila sekta na kuhakikisha maendeleo endelevu yanapatikana jambo linalotimiza kauli mbiu yake ya Kazi Iendelee.

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!