Rais Samia aagiza mkakati wa nishati safi kutafsiriwa kwa lugha mbili

HomeKitaifa

Rais Samia aagiza mkakati wa nishati safi kutafsiriwa kwa lugha mbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya nishati kuhakikisha Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 – 20230 uwe kwa lugha mbili yani kiiswahili na kiingereza ili uweze kueleweka na wananchi wote.

Ametoa agizo hilo wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2024- 2030 uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.

“Ihakikishe inawafikishia makakati huu wadau wote muhimu kwa njia rasmi. Aidha kwa manufaa ya wananchi na wadau wengine kwa ujumla wizara iweke mkakati huu kwenye tovuti yake na kwenye mitandao yake ya kijamii.Mkakati huu utafsiriwe kwa lugha mbili, kiswahili na kiingereza ili wadau wetu wote waweze kuutumia.” amesema Rais Samia

Rais Samia ameitaka wizara hiyo kuhakikisha inakaa chini na wadau husika serikalini na sekta binafsi ili kuweza kuyafahamu maeneo ambayo endapo yatafanyiwa kazi yataongeza kwa uharaka upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa gharama himilivu.

Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa mkakati huo uliozinduliwa leo utanusuru maisha ya Watanzania na kuchochea jitihada za Serikali kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo ukataji miti ambapo hekta 469,000 zinakadiriwa kuteketea kila mwaka.

error: Content is protected !!