Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2024 umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2024. Hii inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2024 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2024.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mwenendo wa kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei wa bidhaa zisizo za vyakula na Core Inflation unachangiwa hasa na misukosuko ya kiuchumi iliyopo Duniani (world economic shocks) kama vile vita baina ya Russia na Ukraine, Palestina na Israel na mabadiliko ya tabianchi ambayo yameathiri sekta mbalimbali na kusababisha uingizaji wa Mfumuko wa Bei kutoka nje (imported inflation) kwa baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zinazoingizwa nchini.
CPI_Apr_2024_Kiswahili