Serikali kuendelea kuiimarisha sekta ya madini

HomeKitaifa

Serikali kuendelea kuiimarisha sekta ya madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuiimarisha sekta ya madini ili iendelee kuwa na manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa mbele ya Soko la Madini katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Akihutubia katika mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Tunduru mkoani Ruvuma, Rais Samia amesema imefanya jitihada kubwa sana ya kuwaonga mkono wachimbaji wadogo wa madini jambo lililochochea ukuaji wa sekta hiyo na mchango wake katika taifa.

“Kupitia STAMICO tumeweza kununua mitambo ya kuchoronga madini inayopelekwa kwa wachimbaji madini na kuongeza uzalishaji wa mapato. Mwaka 2023/24 serikali ilikusanya shilingi bilioni 753 kutoka mapato ya madini ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zimetoka kwa wachimbaji wadogo.” amesema Rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua Soko la Madini katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma

Aidha, Rais Samia amesema serikali itaendelea kuhamasisha uchimbaji wa kisasa kwa wachimbaji wadogo ambao ndio wengi ili wananchi wanufaike zaidi na rasilimali yao.

 

error: Content is protected !!