Panya wa Tanzania Ronin avunja rekodi ya Panya Magawa

HomeKimataifa

Panya wa Tanzania Ronin avunja rekodi ya Panya Magawa

Panya mkubwa wa kiafrika (Cricetomys ansorgei) mwenye jina la Ronin amepata sifa ya kugundua mabomu 109 ya ardhini na vipande 15 vya ziada vya risasi ambavyo haijalipuka alikopelekwa kufanya kazi katika Mkoa wa Preah Vihear, nchini Cambodia.

Hayo yamebainishwa mjini Morogoro katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na uongozi wa shirika lisilo la kiserikali linalofundisha Panya Buku Kutatua Matatizo ya Kibinadamu (APOPO).

Tangu kupelekwa kwake nchini humo Agosti 2021 Ronin amevunja rekodi ya awali ya Panya Magawa akiwa nchini Cambodia aligundua mabomu 71 ya ardhini na vilipuzi vingine (risasi) havijalipuka 38 wakati wa kazi yake ya miaka mitano na alikufa akiwa amestaafu mnamo Januari 2022 na kuleta mafanikio zaidi katika historia ya APOPO iliyopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

 

error: Content is protected !!