Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Ndugu John Mnyika ameufahamisha umma kwamba hatohudhuria na hatoshiriki kwenye kikao cha leo Aprili 12, 2025 kilichoitishwa na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi kikihusisha vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi Mkuu ujao kwaajili ya kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
“Katibu Mkuu sitakuwepo kwenye kikao cha tarehe 12 Aprili 2025 cha kushauriana na kusaini maadili ya uchaguzi ya 2025.”
“Ifahamike kuwa mwenye mamlaka ya kusaini maadili ya uchaguzi kwa niaba ya chama cha siasa ni Katibu Mkuu.”
“Katibu Mkuu sijateua kiongozi au afisa yoyote kwenda kushiriki kwa niaba yangu katika kikao hicho kitakachofanyika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkoani Dodoma.”
Hayo ameyasema leo kupitia ukurasa wake wa twitter (x) ikiwa ni muendelezo wa kushikilia msimamo wa Chama unaoitaka Tume huru ya Uchanguzi kufanya mabadiliko ya usimamizi wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 msimamo huo ukiwa na kaulimbiu ya (No Reform, No Election).