Boti za uvuvi 160 zanunuliwa na Serikali

HomeKitaifa

Boti za uvuvi 160 zanunuliwa na Serikali

Serikali imesema imenunua boti za uvuvi 160 zenye thamani ya sh. bilioni na kuzitoa kwa wanufaika 3,163 nchini.

Hayo yalibainishwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti, alipojibu swali la Maria Kisangi (Viti Maalumu-CCM).

Mbunge huyo katika swali lake la msingi alitaka kujua kuna mpango gani wa kuwawezesha wavuvi wa Kigamboni kwa kuwapa vifaa vya kisasa vya uvuvi.

Akijibu swali hilo, Mnyeti alisema wizara inatekeleza mradi wa kuwawezesha wananchi kupitia dirisha la ECF/IMF kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) tangu mwaka wa fedha 2022/2023.

Mnyeti alisema awamu ya kwanza boti 160 zenye thamani sh. bilioni 11.5 zilitolewa kwa wanufaika 3,163 ambao kati yao idadi ya wanawake ni 1,008 na wanaume 2,155.

Kwa mujibu wa Mnyeti, utoaji wa boti hizo ni endelevu hivyo wizara inahamasisha wavuvi na vikundi vya wavuvi kuendelea kuomba mikopo hiyo wanufaike na fursa hiyo.

error: Content is protected !!