Uzalishaji madini Geita waongezeka kwa 20%

HomeKitaifa

Uzalishaji madini Geita waongezeka kwa 20%

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, mkoa wa Geita umepata mafanikio makubwa yakiwemo kuongezeka kwa uzalishaji wa madini kutoka tani 18.21 mwaka 2021 hadi tani 27.43 sawa na ongezeko la takribani asilimia 20.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shingella alipokuwa akieleza mafanikio ya mkoa huo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu.

“Serikali ya awamu ya sita inatambua kuwa sekta ya madini ina nafasi ya kipekee katika kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni na ukuaji wa uchumi kwa ujumla. Kwa Mkoa wa Geita, Mafanikio yaliyopatikana kutokana na sekta ya madini ni kuongezeka kwa uzalishaji wa madini kutoka tani 18.21 mwaka 2021 hadi tani 27.43 mwaka 2025.” Alisema Shigella.

Shigela ameeleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kusaini mikataba ya kuondoka kwenye matumizi ya ‘Mercury’ katika uchenjuaji wa dhahabu na kwenda kwenye teknolojia ya kisasa kwa lengo la kupunguza athari za afya pamoja na mazingira mpaka kufikia mwaka 2030 pamoja na kuongezeka kwa mitambo ya kisasa ya uchenjuaji dhahabu (CIP) kutoka 10 mpaka kufikia mitambo 25.

Aidha, ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery (GGR)kinachomilikiwa na mzawa, Sarah Masasi mkoani humo ambacho kimesaidia kuongezea thamani dhahabu ya Geita katika Soko la Dunia jambo lililochngia pia kuongezeka kwa fedha za kigeni zilizotokana na uuzaji wa madini kutoka Dola za Marekani 72,878,325.91 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani 92,204,527.35 mwaka 2025 ni moja ya mafanikio hayo.

error: Content is protected !!