Usafiri wa Anga Tanzania wakua kwa asilimia 12.63, abiria wafikia milioni 6.81

HomeKitaifa

Usafiri wa Anga Tanzania wakua kwa asilimia 12.63, abiria wafikia milioni 6.81

Idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini Tanzania imeongezeka kwa asilimia 12.63 na kufikia abiria milioni 6.81 katika mwaka wa fedha 2025/26, ikilinganishwa na abiria milioni 6.037 waliorekodiwa katika mwaka uliotangulia.

Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa, aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma Jumatano, Mei 13, 2026, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Aidha, kiwango cha mizigo iliyosafirishwa kwa njia ya anga katika safari za ndani na nje ya nchi pia kiliongezeka na kufikia tani 34,750.2, ikilinganishwa na tani 33,112.5 zilizorekodiwa katika mwaka wa fedha uliopita.

error: Content is protected !!