Marekani yalegeza makali muswada dhidi ya Tanzania

HomeKimataifa

Marekani yalegeza makali muswada dhidi ya Tanzania

Bunge la Marekani, limeondoa baadhi ya vipengele vilivyotoa masharti makali kuhusu uhusiano wa Taifa hilo na Tanzania, huku moja ya mabadiliko makubwa ikiwa ni kufutwa kwa pendekezo la kusitisha ushirikiano wa usalama na kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Hatua hiyo imebainika katika marekebisho ya Muswada wa S.4577 unaohusu kutathmini upya uhusiano wa Marekani na Tanzania, unaotarajiwa kujadiliwa na Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani Juni 17, 2026.

Mabadiliko makubwa zaidi ni kuondolewa kwa pendekezo la kusitisha ushirikiano wa usalama na kijeshi kati ya Marekani na Tanzania. Rasimu ya kwanza ilitaka msaada wa kiusalama pamoja na fedha za maendeleo vizuiwe, lakini sasa kipengele hicho kimefutwa.

Mbali na kuondoa kipengele cha msaada wa kiusalama, toleo jipya la muswada huo, limeongeza mamlaka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, kuruhusu baadhi ya misaada au uwekezaji wa Marekani kuendelea Tanzania, iwapo hatua hiyo itaonekana kuwa na maslahi kwa taifa hilo.

Muswada huo pia umeongeza mamlaka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuruhusu baadhi ya misaada au uwekezaji kuendelea ikiwa itahitajika kwa maslahi ya taifa la Marekani.

Iwapo utapitishwa na kamati, muswada huo bado utahitaji kupitishwa na Seneti nzima, Baraza la Wawakilishi na hatimaye kutiwa saini na Rais wa Marekani kabla ya kuwa sheria.

error: Content is protected !!