Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imezifungia baa 13 kuendelea na shughuli zake hadi itakapoamuliwa vinginevyo, kwa kukikiuka masharti ya Sheria ya Leseni za Biashara ya Vileo ya mwaka 1968 baada ya kupokea malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kuhusu kelele za muziki unaopigwa katika baa hizo.
Akizungumza na vyombo vya habari, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Vileo ya mwaka 1968 na itakuwa endelevu ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira salama na yenye utulivu.
Mnyonge amesema miongoni mwa baa zilizofungiwa ni;
Tips Mikocheni
Elements
Polos
Babylon Corner
Kwa Joyce Cosmas
Serengeti Bar Makumbusho
Big Joe
Otea Bar Msasani
Velvet Club
Rafael Kajubiri Makumbusho
Uncles
Tips Coco Beach
Bikers Lounge Bunju
Amesema kutokana na wingi wa wateja, magari na pikipiki hujazana hadi katika maeneo ya makazi ya watu, jambo linalowasumbua wakazi wanaporejea majumbani mwao.


