DCI akataa kutoa ushahidi kesi ya Lissu

HomeKitaifa

DCI akataa kutoa ushahidi kesi ya Lissu

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai, amekataa kutoa ushahidi mahakama katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Kutokana na hali hiyo, Lissu ameiomba mahakama iruhusu upande wa utetezi kufunga ushahidi wake, akisema hawezi kuwalazimisha mashahidi hao kutoa ushahidi.  Pia ameomba mahakama ipange tarehe maalum kwa ajili ya kusikiliza hoja za mwisho za pande zote mbili.

Upande wa mashtaka umeunga mkono ombi hilo, huku ukiitaka mahakama kufafanua iwapo hoja za mwisho zitawasilishwa kwa njia ya mdomo au maandishi.

 

error: Content is protected !!