Matunda ya Royal Tour

HomeKitaifa

Matunda ya Royal Tour

Filamu ya Royal Tour pamoja na ziara za Rais Samia Suluhu Hassan nje ya nchi, zimefungua uchumi wa Tanzania kwa kuongeza uwekezaji kutoka Dola za Marekani bilioni 1 sawa na sh trilioni 2.3 mpaka kufikia Dola bilioni 9.2 sawa na trilioni 21.16.

Pia mauzo ya nje yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 10 sawa na Sh trilioni 23 kutoka dola za Marekani bilioni 7.

Akizungumza katika mkutano wa mafanikio ya ziara ya Rais Samia nchini Oman uliofanyika leo Juni 28,2022 Ikulu, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Godius Kahyarara, amesema kuongezeka kwa mapato hayo ni hatua nzuri, kwani inaongeza watalii wengi na kuongeza mauzo ya nje ambayo yatasaidia kupunguza ukali wa deni la taifa.

Amesema pia, tathmini ya serikali kuanzia Machi 21 hadi Juni 25, 2022, serikali imeweka lengo la kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi na kufikia asilimia 30 ya Pato la Taifa (GDP) ifikapo mwaka 2025.

error: Content is protected !!