Bashungwa awala vichwa wakuu wa ugavu 23

HomeKitaifa

Bashungwa awala vichwa wakuu wa ugavu 23

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe kuwashushwa vyeo wakuu 23 wa vitengo vya manunuzi na ugavi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini.

Wakuu wa vitengo walihusika ni wa Halmashauri za Arusha CC, Monduli DC, Dodoma CC, Geita TC, Geita DC, Kyerwa DC, Kigoma DC,Same DC, Siha DC, Butiama DC,Busekelo DC,Kyela DC, Mbarali DC, Mvumero DC, Mwanza CC, Buchosa DC, Chalinze DC, Kisarawe DC, Mkuranga DC, Itigi DC, Korongwe DC, Handeni TC na Pangani DC.

Taarifa hiyo ilibainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Nteghenjwa Hosseah kupitia vyombo vya habari jana na kusema hatua hiyo ilikuja ya Waziri Bashungwa kutoa maagizo hayo baada ya tathmini iliyofanyika ya utendaji kazi kwa baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kama ilivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu wakati wa ziara yake mkoani Maara mwezi uliopita.

“Tathmini ya utendaji kazi wa Wakuu wa Vitengo vya Manunuzi na Ugavi imefanyika ili kubaini utendaji kazi wa watumishi hao katika kusimamia masuala mbalimbali ya ununuzi wa Umma. Baada ya tahmini hii kukamilika katika kitengo cha Manunuzi na Ugavi hatua mbalimbali zimechukuliwa zenye lengo la kuimarisha utendaji kazi,” alisema Hoseah.

 

error: Content is protected !!