Polisi kuwakamata wanaohamasisha vurugu

HomeKitaifa

Polisi kuwakamata wanaohamasisha vurugu

Jeshi la Polisi nchini limesema kumekuwepo na mipango, matamko na uhamasishaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa dini, siasa na wanaharakati kisirisiri kupitia vikao vya ndani na uhamasishaji wa wazi wenye nia ya kuhamasisha watu kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misiime imesema vitendo hivyo vya kihalifu vinavyopangwa ni pamoja na kufanya vurugu, kuharibu miundombinu inayotumiwa kutoa huduma kwa umma, mali za umma na binafsi.

Aidha, Jeshi hilo limesema linaendelea kufuatilia kwa karibu mipango hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, huku likitumia taarifa inazopokea kubaini na kuwakamata wanaohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.

error: Content is protected !!