Serikali: Tutaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya CAG

HomeKitaifa

Serikali: Tutaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya CAG

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inaendelea kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya ubadhirifu.

Amesema hayo Novemba 6, 2026, wakati akiwasilisha hotuba ya kuahirisha bunge ambapo amewakumbusha Maafisa Masuuli na watendaji wote wa Serikali kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za umma kwa mujibu wa mipango na bajeti, ili kuepusha hoja za ukaguzi na upotevu wa fedha.

Amesema wabunge wamechangia kwa hisia kubwa, wakionesha namna walivyo na uchungu na rasilimali za Taifa.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu amezitaka wizara na taasisi zote kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, tarehe 30 Oktoba, 2026.

error: Content is protected !!