HomeKimataifa

Yafahamu Magereza 10 yenye starehe zaidi Duniani

Ukifiria gereza/jela, ni aghalabu sana kufikiria starehe na anasa ndani yake. Lakini Dunia haijawahi kuacha kutushangaza kila uchwao. Haya hapa magereza 10 duniani ambayo watu wake wanaishi kama au pengine kuliko hata zaidi ya uraiani.

1. Bastoy Prison, Norway
Gereza hili lipo Kisiwa cha Oslofjord ambapo inakadiriwa watu linaweza kufunga watu wasiozidi 150. Ndani ya Gereza hilo unaweza kucheza “Tennis”, kuendesha farasi, kuvua samaki na makazi mazuri kabisa. Wafungwa hufanya kazi nyepesi na pia hakuna ulinzi mkali. Inaelezwa kuwa wafungwa kwenye Gereza hili kuna muda husahau kuwa wao ni wafungwa.

2. HMP Addiewell, Scotland
Gereza hili lina wafungwa 700 tu, na kila wiki kuna saa 40 ya kujifunza ujuzi mbalimbali na pia kujifunza namna gani ya kuishi vizuri na jamii pindi kifungo kitakapokwisha.

3. Otaga Corrections Facility, New Zealand
Gereza hili kwanza lina ulinzi wa kutosha, lakini lina vyumba vizuri, vikubwa na vyenye mahitaji muhimu. Gereza hili halina kazi ngumu kabisa, bali wanaamini kuwa namna ya kubadili tabia ya mtu ni kumfundisha stadi za maisha. Wafungwa hufundishwa uhandisi, upishi na pia ufugaji.

4. Justice Centre Leoben, Austria
Gereza hili wafungwa hupewa chumba chenye choo ndani, luninga na jiko dogo. Halafu nje kuna sehemu ya mazoezi ya jumuiya, uwanja wa mpira wa kikapu na starehe nyingine kama kuogelea.

5. Aranjuez Prison, Spain
Wakati magereza mengi duniani hutenga wafungwa na familia zao, gereza hili humruhusu mfungwa kuishi na mtoto wake ndani ya Gereza hilo kwa mwaka mmoja. Gereza hilo lina mahitaji yote muhimu ya mtoto na pia linampa mtoto fursa ya kujifunza hali ya gerezani ilivyo.

6. Champ – Dollan Prison, Switzeland
Vyumba vya Gereza hili vinafananishwa na mabweni ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo, kwani vina mahitaji yote muhimu kama choo binafsi, shelfu ya vitabu, kitanda kizuri na shuka safi zinazobadilishwa mara kwa mara. Pia chakula katika Gereza hili ni kizuri kama kile cha migahawa mingi mikubwa nchini humo.

7. JVA Fuhlsbuettel Prison, Germany
Vyumba vya Gereza hili vina mashine ya kufulia nguo, makochi na bafu binafsi. Vumba vyake havina giza, vina madirisha mapana yanayoingiza hewa na mwanga wa kutosha, hivyo humpa mfungwa hali ya kujihisi vizuri. Humo Gerezani pia kuna vyumba vya mikutano na sehemu za starehe kama kuogelea.

8. Sollentuna Prison, Sweden
Wafungwa huwekwa kwenye vyumba vyenye vyoo ndani, vifaa vya mazoezi, jiko binafsi, runinga pamoja makochi yenye mito laini. Mfungwa anaweza kutumia vifaa vya muziki kama gitaa na vinginevyo kwa kadiri ya mahitaji yake.

9.Halden Prison, Norway
Gereza hili limezungukwa uoto mzuri na pia liko katika eneo ambao kuna mwanga wa kutosha. Gereza hili limepewa sifa ya kuwa gereza linalojali zaidi maisha ya binadamu na hii ni kwa sababu wafungwa wanaweza kucheza michezo mbalimbali, kuna vipindi vya mafunzo, kufuatilia vipindi vya runinga kwa uhuru, sehemu za mazoezi, vifaa vya kunakili muziki na kila ambacho mfungwa anataka kutimiza ndoto zake ndani ya Gereza.

10. Cebu Prison, Phillippines
Gereza hili halina anasa nyingi kama magereza ambayo yametangulia, lakini kwenye gereza hili mfungwa anaweza kushiriki mazoezi ya kuimba, kucheza muziki na pia watu kutoka uraiani hualikwa gerezani humo kutazama maonesho ya muziki ya wafungwa hao. Watu wanaotoka uraiani mara nyingine hulazimika kulipia viingilio kuingia gerezani humo kutazama maonesho mbalimbali.

error: Content is protected !!