Kutokana na ukweli kwamba mpira wa miguu ndio mchezo wenye mashabiki wengi zaidi ulimwenguni, wadhamini mbalimbali hutoa fedha nyingi kwa ajili ya kujitangaza kupitia timu hizo.
Ifuatayo ni orodha ya timu za soka 10 zinazopata fedha nyingi zaidi kutoka kwa wadhamini wanaoweka chapa au majina yao mbele kabisa kwenye jezi za timu hizo:
10. Juventus
Mdhamini mkuu wa timu hiyo ya Italia kwa sasa ni kmapuni ya magari, Jeep. Jeep na Juventus wana mkataba unaotarajiwa kufikia ukomo mwaka 2022/2023 huku thamani yake ikiwa dola za Kimarekani 159.
9. Chelsea
Mbele ya jezi za Chelsea ya Uingereza kuna chapa inayoonekana kamba namba 3. Hiyo ni chapa ya wadhamini wakuu wa timu hiyo kwa sasa, kampuni kutoka Uingereza iitwayo ‘Three’ inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano. Mkataba wa Three na Chelsea utadumu hadi 2024 na una thamani ya dola za Kimarekani 166.
8. Paris Saint Germain (PSG)
Ni timu ya soka kutoka Ufaransa inayodhaminiwa na taasisi ya kifedha ya Accor, kupitia mkataba unaotarajiwa kukamilika msimu huu. Udhamini huo una thamani ya dola za Kimarekani 171.
7. Liverpool
Mkataba wa Liverpool ya Uingereza na benki ya Standard Chartered unaotarajiwa kudumu hadi msimu wa 2022/2023 una thamani ya dola za Kimarekani 221.
6. Arsenal
Jina la shirika la ndege kutoka falme za Kiarabu, Emirates, linatonekana kwenye jezi za Arsenal hadi msimu wa 2023/2024, kupitia mkataba wenye thamani ya dola za Kimarekani 280.
5. Bayern Munich
‘Deutsche Telekom’ (T-Mobile) wana mkataba na Bayern Munich ya Ujerumani. Mkataba utakwenda hadi 2022/2023 na una thamani ya dola 283 za Kimarekani.
4. Barcelona
Rakuten ni kampuni ya Japan inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali kupitia mtandao. Kampuni hiyo inaidhamini Barcelona ya Hispania kwa dola za Kimarekani 324 kupitia mkataba utakaofikia tamani mwishoni mwa msimu huu.
3. Manchester United
Mkataba wa ‘Mashetani Wekundu’ kutoka Uingereza na kampuni ya vifaa vya kielekroniki ya ‘Team Viewer’ una thamani ya dola za Kimarekani 325 na utatamatika mwaka 2026.
2. Tottenham
American International Assurance (AIA) wataidhamini Tottenham ya Uingereza hadi mwaka 2027. Mkataba wao una thamani ya dola za Kimarekani 400.
1. Real Madrid
Emirates, shirika la ndege kutoka falme za Kiarabu, linaidhamini Real Madrid ya Hispania. Mkataba wao unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa msimu huu una thamani ya dola za Kimarekani 413.