Wanawake wengi wanapitia chanagamoto za ugomvi kwenye ndoa zikihusuishwa na mama wakwe utajuaje kama mama mkwe wako hakupendi hizi hapa ni ishara aza kutambua mama mkwe wako hakupendi;
1. Kukupa pongezi za uongo
Unakuta mkwe wako anakusifia kwenye kila kitu mwanzoni unaweza usijue kuwa anakukejeli lakini ukichunguza kwenye pongezi anazokupa utakuta ni sifa za uongo.
2. Atakupa changamoto kwenye kila unachokifanya
Ikitokea umeongea chochote lazima na yeye aongee ila sio kwa nia nzuri ataongea ili kukufanya upate hasira na ujibizane nae hususani mbele za watu ili udharirike.
3. Kuongelea vibaya sehemu unapotoka
Muda wote atakua anaongelea vibaya sehemu uliotoka inaweza kuwa kabila, mahali ulipozaliwa au ulipoishi hii akimaanisha hajakukubali na hivyo vyote anavyoongea ni anakulenga wewe.
4. Atakwambia maneno ambayo mwenzi wako amaemwambiaUkikaa nae atakupa taaarifa amabazo alizungumza na mtoto wake kuhusu wewe hii itakufanya ukose ujasiri na kutokumwani mwenzi wako.
5. Kuongelea wanawake waliowahi kuwa na mahusiano na mtoto wake
Mama mkwe kuwaongelea wasichana waliowahi kuwa na mtoto wake ni ishara ya kwamba hakueshimu na hawezi kuwasahau hao wasichana, unachotakiwa kufanya ni kutokukubali hali hiyo isikusumbue.
6. Kutokukualika katika shughuli za familia
Unapoolewa ni moja kwa moja unakuwa mwanafamilia kwenye familia ya mumeo hivyo mkweo anatakiwa kukualikua na kukujulisha kwenye matukio yanayoendelea kwenye familia kama mkweo hafanyi hivyo maanake ni hakupendi.
7. Atakuletea zawadi za kutibu kasoro zako
Kama una hunusi atakuletea dawa ya chunusi, kama ni mnene atakupa dawa za kupunguza unene sio kama anafanya hivyo ili kukusaidia ila anakua anazungumza kwa ishara kuwa hapendezwi na wewe