Miaka 90 ya Desmundu Tutu na kumbukizi ya Sera ya Kibaguzi Afrika Kusini

HomeElimu

Miaka 90 ya Desmundu Tutu na kumbukizi ya Sera ya Kibaguzi Afrika Kusini

Askofu Desmond Mpilo Tutu alizaliwa Oktoba, 7 1931 katika mji wa Klerksdorp Afrika Kusini. Wazazi wake walitoka makabila ya Xhosa na Tswana na akiwa mdogo alipata bahati ya kusoma katika Shule ya Kanisa ambayo Baba yake mzazi alikuwa Mwalimu.

Desmond akiwa mtoto alihusudu sana kuwa Daktari lakini bahati mbaya sana gharama za masomo zilimshinda na hatimaye akaangukia kuwa Mwalimu mnamo mwaka 1955. Miaka miwili baadae (1957) Desmond aliacha kazi hiyo na kujiunga na Chuo cha dini cha Mtakatifu Peter jijini Johannesburg na akatawazwa kuwa Askofu mwaka 1961.

Mwaka 1962 alitunukiwa Shahada ya pili kutoka ‘King’s College’ London Uingereza. Kati ya 1972 na 1975 alifanya kazi kama Mkurugenzi Mwandamizi wa baraza la makanisa duniani ambapo 1975 Desmond alikuwa mtu mweusi wa kwanza  nchini Afrika Kusini kushika wadhifa wa ukuu wa Chuo Kathedro ya Mtakatifu Maria kilichopo jijini Jonannesburg.

    >Historia: Mtanzania ashinda Tuzo ya Nobel

1978 Desmond alikubali uteuzi kuwa Katibu Mkuu Baraza la Makanisa, Afrika Kusini na kuwa mzungumzaji mkubwa wa haki za watu weusi Afrika ya Kusini. 1980 Destmund alikuwa kinara kwenye kufichua madhila ya mateso ya sera za kibaguzi kwa dunia nzima.

Desmund si muumini wa umwagaji damu katika kudai haki, mara zote alihusia kudai haki kwa njia ya amani na majadiliano, ambapo aliomba Jumuiya za Kimataifa kuwekea vikwazo vya kiuchumi Serikali ya Afrika ya Kusini ya wakati huo ili kukomesha vitendo vyake vya kinyama dhidi ya watu weusi.

Mwaka 1984 Desmond anashinda tuzo ya Nobel wakati ambao Afrika ya Kusini ilikuwa kwenye kilele cha vurugu za kupiga sheria za kibaguzi, tuzo hii inakuwa alama ya Jumuiya ya Kimataifa kuionesha Dunia kuwa haiuingi vitendo vya Serikali ya kikaburu nchini Afrika ya Kusini. Mwaka 1986 Desmond akatawazwa kuwa askofu wa kwanza mweusi katika Jiji la Cape Town.

Desmund Tutu ameandika na kuhusika kwenye uandishi wa vitabu kadhaa kama vile ’Divine Intention (1982), ’Hope and Suffering (1982), No Future without Forgiveness (1999) na vingine vingi.

error: Content is protected !!