Ijue Tuzo ya Nobel na namna ya kushiriki

HomeKimataifa

Ijue Tuzo ya Nobel na namna ya kushiriki

Tuzo ya Nobel ni tuzo ya heshima na ya hadhi ya juu inayotunukiwa kwa watu ambao wametoa mchango mkubwa sana katika katika kufanya uvumbuzi au kuanzisha jambo ambalo limechangia sana katika maisha ya binadamu.

Tuzo ya kwanza ya Nobel ilitolewa mwaka 1901, takribani miaka 120 iliyopita. ‘Nobel’, jina linalotokana na mwasisi wa tuzo hiyo, Alfred Nobel ambaye aliacha usia nnamo 1891 kuwa tuzo hizo zitolewe kwa watu ambao mwaka mmoja nyuma, walifanya mambo makubwa yenye mchango kwa maisha ya binadamu.

Tuzo ya Nobel ina vipengele sita vinavyoshindaniwa, navyo ni Fizikia, Kemia, Saikolojia au Tiba, Fasihi, Amani na Uchumi. Kwa lugha ya kimombo tuzo hiyo hujulikana kama “Nobel Prize”, lakini katika nyaraka rasmi tuzo hii huitwa “The Sveriges Riksbank Prize in Economic Sciences in Memory of Alfred Nobel”

Mtu anateuliwaje na kushinda tuzo ya Nobel?

Mwaka 2021 watahiniwa 329 waliingia katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo, 234 ikiwa ni watu binafsi na 95 ikiwa na mashirika. Majina ya watahiniwa na wale waliopendekeza watahiniwa hawa, hayatotoka hadharani hadi ipite miaka 50.

Hakuna sehemu ya kuomba kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho, bali mgombea lazima apendekezwe na mapendekezo lazima yawe na masharti yafuatayo.

> Historia: Mtanzania ashinda tuzo ya Nobel

1. Mapendekezo lazima yatoke kwa wabunge au mawaziri wa serikali ya nchi huru au Rais wa nchi husika.
2. Mapendekezo yatoke kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ‘The Hague’ na Mahakama kuu ya Usuluhishi ya ‘The Hague’
3. Mapendekezo yatoke taasisi ya Sheria za Kimataifa (Members of l’Institut de Droit International
4. Mapendekezo yatoke Taasisi ya Kimataifa ya wanawake inayohusu maswala ya amani na uhuru
5. Wahadhiri wa vyuo vikuu hasa wa ngazi ya Profesa katika vitivo vya Historia, Sayansi ya Siasa, Sheria, Dini, na Falsafa. Katika mrengo huo huo, pia mapendekezo yanaweza kutoka kwenye kituo utafiti na taasisi zinazohusu maswala ya sera za mambo ya nje.
6. Pia mapendekezo yanaweza kutoka kwa mtu ambaye amewahi kushinda tuzo ya Nobel.
7. Mapendekezo yatoke kwa taasisi ambayo imewahi kutunukiwa tuzo hiyo.
8. Mapendekezo yanaweza kutoka pia kwa mwanajopo aliyopo au aliyepita wa kamati maalumu ya kupitisha majina ya washindi. Mwanakamati anapaswa kupeleka jina mapema zaidi kabla ya kikao cha kwanza cha kamati cha Februari 1.
9. Washauri waliopita wa kamati ya tuzo ya Nobel.

Ni lazima mshiriki apendekezwe na moja ya asasi au watu walioanishwa hapo huu, hakuna njia ya kujipendekeza

– Kamati ya Nobel ina watu watano wanachaguliwa kutoka Bunge la Norway na tuzo hiyo hutolewa Mji Oslo nchini Norway.

  • Utaratibu wa kumpata mshindi unakuwaje?
  • Septemba 1 – Kamati inapokea majina ya watu waliopendekezwa
  • February 31 – Ni mwisho wa kutuma majina ya wanapendekezwa
  • Machi 3 – Majina ya wanaoshindanishwa yanakuwa yameshapatikana
  • Mei – Septemba – Kamati kupitia majina ya washindi baada ya kupiga kura
  • Octoba 5 – Baada ya kura matokeo ya kura yanatangazwa
  • Octoba 6/7 – Mshindi wa Tuzo ya Nobel anatangazwa
error: Content is protected !!