TCU yaongeza muda wa udahili

HomeKitaifa

TCU yaongeza muda wa udahili

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Charles Kihampa ameeleza kuwa nyongeza ya muda wa udahili kuanzia Ijumaa hii imekuja baada ya kukamilika kwa udahili katika awamu Tatu za awali.

Akizungumza na waandishi wa habari Profesa Kihampa ameeleza kuwa muda umeongezwa Ili kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakudahiliwa au hawakuweza kuomba udahili katika awamu Tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali.

“Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua awamu ya Nne na ya mwisho ya udahili inayoanza Oktoba 11 hadi oktoba 15, 2021.” alisema Profesa Kihampa.

Profesa Kihampa amefafanua kuwa baada ya awamu Tatu za awali kukamilika wamekua wakipokea maombi mengi kutoka kwa wadau mbalimbali vikiwamo vyuo na Taasisi za Elimu ya juu wakiomba kuongezewa muda wa udahili kwa ajili ya waombaji waliokosa udahili kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha amewasisitiza waombaji na Vyuo vyote kuzingatia utaratibu wa udahili katika awamu ya Nne kwa mwaka wa masomo ujao na ratiba inaonesha kuwa, Oktoba 11 hadi 15, mwaka huu, ni siku za kutuma maombi ya udahili na Oktoba 19 hadi 20, 2021, ni muda wa Vyuo kuwasilisha majina ya waliodahiliwa katika awamu ya Nne kwa TCU. #clickhabari

error: Content is protected !!