Tarehe na mwezi kama wa leo (Oktoba 16) mwaka 1945, Shirika la chakula duniani (FAO) liliasisiwa. Shirika hilo ambalo hati ya kuasisiwa kwake lilipitishwa katika mji wa Québec nchini Canada lilianzishwa kwa lengo la kuzisaidia nchi wanachama kukusanya taarifa, ripoti na takwimu zinazohusiana na chakula, kilimo, utunzaji wa misitu na uvuvi na kufanya tathmini kuhusu uzalishaji wa chakula.
Malengo mengine ni pamoja tathmini kuhusu ugavi wa chakula duniani na juhudi za kuboresha uzalishaji, masoko ya chakula, kulinda maliasili, kupanga sera zinazohusiana na kilimo na chakula n.k
Kufuatia kumbumbuku hiyo tarehe 16 Oktoba kila mwaka inatambulika kama Siku ya Kimataifa ya Chakula.