Patson Daka: Mzambia aliyepeleka kilio Trafford

HomeMichezo

Patson Daka: Mzambia aliyepeleka kilio Trafford

Patson Daka (23) alisajiliwa na klabu ya Leicester City kwa dau la Euro Milioni 23 kutoka klabu ya Salzburg nchini ya Austria. Daka kabla ya kujiunga na Leicester kwenye dirisha la usajili julai mwaka huu, ameifungia klabu yake ya Red Bull Salzburg magoli 34 kati ya michezo 42 aliyochezea na kusaidia klabu yake kutwaa kikombe cha Ligi kuu Austria.

Daka amesaini kandarasi ya miaka mitano kukipiga katika klabu ya Leicester City.

Katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa leo uwanja wa King Power katika ya Leicester City na Manchester United, Daka aliingia dakika ya 77 akipishwa na Kelechi Ihenacho. Dakika ya 91 Daka alifunga goli kutoka kwenye mpira wa adhabu wa faulu iliyopigwa Ayoze Perez nje kidogo ya eneo la kumi na nane.

Amefunga goli la nne katika mchezo ulioisha wa goli 4 kwa 2 ambacho Manchester United imepoteza mchezo huo, na kumfanya kutokushinda michezo mitatu mfululizo ya Ligi Kuu ya England.

Daka anaweka rekodi kuwa raia wa kwanza wa Zambia kufunga goli katika Ligi Kuu England. Ligi hiyo ina ina wachezaji wawili tu raia wa Zambia, Daka wa Leicester pamoja na Enock Mwepu wa Brighton & Hove Albion.

error: Content is protected !!