Huu ni mlo wa chap chap hasa pale asubuhi unapotaka kupata kifungua kinywa kabla ya kwenda kwenye mihangaiko yako ya kila siku.
Mahitaji:
- Soseji pakiti 1
- Mayai 5
- Nyanya 3
- Vitunguu maji 2
- Majani ya mint kiasi
- Pilipili manga
- Pilipili hoho 1
- Chumvi
Maelekezo:
- Pasua mayai yako kwenye bakuli safi yachanganye
- Kwenye hilo hilo bakuli kata kata soseji zako saizi unazopendelea
- Katia hoho kidogo
- Katia vitunguu nyembamba
- Katia nyanya ziepuke mbegu za nyanya
- Nyunyuzia pilipili manga na chumvi
- Dondoshe majani kidogo ya mint
- Changanya kwa pamoja
- Weka kikaangio jikoni na mafuta kiasi
- Mimina mchanganyiko wako
- Ukaushe vizuri kama unavyokausha mayai
Baada ya hatua zote hizo soseji zako za mayai zipo tayari unaweza kunywea chai, juisi, soda au hata maji.