Burna Boy na Mama yake washutumiwa kwa utapeli

HomeBurudani

Burna Boy na Mama yake washutumiwa kwa utapeli

Promota wa muziki anayeishi Marekani Emmanuel Chinyere Uzoh amemshutumu Mshindi wa tuzo ya Grammy, Burna Boy pamoja na Mama yake mzazi Bose Ogulu kwa makosa ya wizi, ulaghai pamoja na utapeli.

Uzoh ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gold Mool Entertainment, amesema kuwa Burna Boy alilipwa kiasi chote cha fedha alichohitaji, lakini  haelewi kwa nini hakutokea kutumbuiza.

> Uchambuzi wa kina kuhusu ubora na udhaifu wa Yanga

Kupita ukurasa wa Instagram wa kampuni ya Gold Mool Entertainment, Uzoh alisema kuwa Mama yake Burna ambaye ni meneja wa msanii huyo, alitaka kuchukua shilingi milioni 20 kwa njia za kitapeli kutoka kwao.

Burna Boy licha ya kulipwa shilingi milioni 30 kutokea kwenye moja ya kumbi ya starehe kutuimbia nchini Marekani, lakini hakutokea. Uzoh amesema kuwa amejaribu sana kuongea na uongozi wa Burna kutaka kurudishiwa fedha zake, lakini uongozi wa Burna umeonesha ukaidi kwenye hilo. Uzoh anadhamira kuchukua hatua za kisheria muda wowote.

error: Content is protected !!