Utata wazuka waliofariki ajali ya moto, marehemu adaiwa mahari

HomeKitaifa

Utata wazuka waliofariki ajali ya moto, marehemu adaiwa mahari

Mume na Mke ambao ni miongoni wa watu watano wa familia moja waliofariki kutokana na ajali ya moto mwanza wamezikwa maeneo tofauti kutokana na Mwanaume kutolipa mahari, Lameck Benedicto alizikwa nyumbani kwao katika Kitongoji cha Misungwi wilaya ya Shinyanga na mazishi ya Mkewe Leah Lameck na mtoto wake Eunice Lameck yanatarajia kufanyika Mtaa wa Ndala Wilayani Shinyanga.

Mwenyekiti wa mtaa wa Igoma Mashariki Michael Mhangwa anasema “Kutokana na mila na desturi, familia ya mwanamke ilichukua mwili wa mtoto wao pamoja na mjukuu na kwenda kuwazika kwa sababu mwanaume hakuwa amelipa mahari. Kwa mujibu wa mila na desturi ya kisukuma mwanamke anazikwa kwenye eneo la familia ya mumewe pale tu mwanaume anapomaliza kulipa mahari”

Katibu Mkuu wa machifu wa jamii ya kisukuma Aaron Mikomangwa anasema kutoa mahari na kupokelewa ni ishara ya mwanaume kukubalika na wakwe zake, ni utaratibu wa kimila na desturi mwanaume asiyemlipia mahari mke wake anakosa haki za msingi juu ya mke huyo ikiwemo kumzika.

Sambamba na hilo Mikomangwa aliomba jamii kuendelea kuenzi, kuheshimu na kuendeleza mila na desturi nzuri zinazolinda haki na heshima ikiwemo ya mwanaume kutoa mahari kwa wazazi wa mwanamke kama sehemu ya asante na kuunganisha udugu.

error: Content is protected !!