Dk. Janabi: Ugonjwa wa presha unapunguza nguvu za kiume 

HomeElimu

Dk. Janabi: Ugonjwa wa presha unapunguza nguvu za kiume 

Mkurugenzi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohammed Janabi amesema ni kweli kwamba dawa za presha zinapunguza nguvu za kiume lakini ugonjwa wenyewe wa shinikizo la juu la damu unasababisha zaidi ukosefu wa nguvu za kiume na kusisistiza kwamba endapo mtu atatumia dawa na kuona zinamletea shida hiyo ni vyema ukarudi kwa daktari wako akakubadilishia dawa.

“Ni kweli , lakini si dawa zote za presha au za moyo zinapunguza nguvu za kiume, kama kuna dawa umekunywa na ukaona athari yake ni kupungua kwa nguvu za kiume basi ni vyema kurudi kwa Daktari wako akakubdilishie , lakini kubwa zaidi ugonjwa wenyewe wa shinikizo la damu unapunguza nguvu za kiume mara mia zaidi, presha tu inatosha kukupunguza nguvu za kiume.” Amesema Dk. Janabi.

Dk. Janabi pia ameeleza kuwa endapo utagundulika kwamba una ugonjwa wa shinikizo la damu au presha ni vyema ukazingatia kunywa dawa kwa wakati sahihi kwani dawa hizo inabidi uwe unakunywa kila siku bila kukosa kwa sababu matibabu yake ni maisha.

error: Content is protected !!