Rekodi mpya yavunjwa Bandari ya Dar

HomeKitaifa

Rekodi mpya yavunjwa Bandari ya Dar

Ni mwezi mmoja umepita tangu Bandari ya Dar es Salaam kuvunja rekodi ya kupokea meli kubwa yenye magari 4,041, jana rekodi mpya imevunjwa baada ya meli nyingine kubwa ya Meridian Ace kuingia ikiwa na magari 4,397.

Bandari hiyo imeanza kufanya kazi kwa kiwango cha juu cha kimataifa baada ya kufanyiwa maboresho makubwa kwa ujenzi wa gati za kisasa.

Nicodemus Mushi, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA) alisema ujio wa meli hiyo ni matokea ya kazi kubwa ya kuziwezesha na kutangaza uwezo wa Bandari za Tanzania, kulikofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tangu ameingia madarakani Rais Samia amekuwa balozi namba moja wa huduma za bandari, jukumu ambalo analifanya sambamba na wasaidizi wake wakuu, jitihada ambazo sasa zimeanza kuzaa matunda,” alisema Mushi.

Mushi alisema pia kwamba, Meridian Ace(IMO:9209518) iliyojengwa miaka 22 iliyopita ikiwa ni meli ya kubeba magari ina urefu wa mita 199.94 na upana wa mita 32.2 ilikuwa imebeba magari 4,397, magari 3,406 yanavuka mipaka na 911 yanabaki nchini.

error: Content is protected !!