Mahusiano ya mbali yanaweza kuwa magumu kwa baadhi ya watu, wengi wameishia kulia kutoka na mahusiano ya namna hii. Lakini japo ya changamoto zake, zipo njia kadhaa kama zitafuatwa vizuri basi zinaweza kusaidia penzi la mbali kuweza kudumu. Njia zenyewe ni kama zifuatazo,
1. Wasilianeni mara kwa mara
Kutokana na teknolojia iliokuwepo mawasiliano yamekua rahisi hata kama mko katika nchi tofauti, mnaweza kuwasiliana kwa kupigiana simu, kutumiana ujumbe mfupi wa maneno au kwa kupigiana kwa njia ya video. Ni vizuri zaidi mkiwa mnawasiliana huku mnaonana kwani inasaidia pia kuona hisia za mwenzi wako katika macho yake au ishara anazotumia pia inasaidia kudumisha mvuto wa mwenzi wako kwako.
2. Tembeleaneni
Kama sehemu ambayo mwenza wako yupo unaweza kwenda ni vyema kumtembelea mara kwa mara unapopata nafasi, unapomtembelea mpenzi wako itasaidia kuimarisha mahusiano yenu na itamfanya mara zote akumbuke kwanini aliamua kuwa na wewe na uendapo kumtembela jaribu kutengeneza kumbukumbu ambayo itamfanya atamani uwe unaenda muda wote, mfano kumsaidia kufanya shughuli zake, ongea nae mfanye afurahi lakini pia mnaweza kupiga picha.
3. Muamini mwenzi wako
Ukweli ni kwamba ni rahisi mmoja wenu kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano ya mbali, mwingine huchanganyikiwa kuwaza kutaka kujua mpenzi wake muda huu anafanya nini na yuko na nani kama una imani haba na mpenzi wako. Hali hii inaweza kukupelekea kupiga simu kila wakati, au kutuma meseji nyingi sababu tu ya kukosa kumwamini mwenzi wako. Kama una tabia ya kutokwa na imani na mpenzi wako mara kwa mara, jiulize kwanini. Kama sababu ni ikiwa awali uliwahi kusalitiwa, huna budi kujifunza kisha kusahau hayo mambo. Imani ni msingi imara sana katika mahusiano yoyote,
4. Kuwa muwazi
Katika mahusiano ya mbali ni rahisi sana kwa mmoja wenu kuwa msiri sana kwa mwenzie, lakini uwazi ndio kitu kikachofanya mahusiano yenu yaendelee kuwa hai, Kwenye vitu vyako unavyofanya mshirikishe na hata hisia unazopata mwambie kama umemkumbuka mwambie ili ajue kwamba bado una upendo nae na katika safari yenu bado mko pamoja.
5. Weka mipaka
Hata kama mwenzi wako yuko mbali kumbuka maisha lazima yaendelee hivyo usijibane sana kwa kukaa sana nyumbani, Kama una marafiki zako nenda kawasalimie kama kuna sehemu unapenda kwenda kwaajili ya starehe pia unaweza kwenda ila unatakiwa tu kuwa makini na uwe na mipaka kwamba uko kwenye mahusiano hata kama utaenda huko utajiheshimu na hata kama una rafiki wa kiume hautaruhusu mazoea yaliyopitiliza.