Rais Samia akaribisha wawekezaji zaidi nchini

HomeKitaifa

Rais Samia akaribisha wawekezaji zaidi nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi wawekezaji kuja na kuwekeza nchini kwakuwa serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ufanyaji wa biashara na uwekezaji kwani sekta binafsi huleta mageuzi makubwa katika kuinua uchumi wa taifa.

“Ndugu zangu mabibi na mabwana, serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ufanyaji wa biashara na uwekezaji. Tunafahamu bila mchango wa sekta binafsi hatuwezi kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa nchi yetu.” – Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Mapendekezo 4 ya Bunge kumaliza sakata la machinga

Amezungumza hayo akiwa katika uzinduzi wa kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani huku akisisitiza kwamba  wawekezaji wapewe nafasi ya kufanya uwekezaji nchini kwani endapo watacheleweshwa na kutopewa maeneo basi hata nchi nayo itakosa bahati yakuwa na wawekezaji hao.

“Tunapomchelewesha mwekezaji, unachelewesha ajira kwa vijana wetu, unachelewesha kodi na unadumaza uchumi wa Taifa letu. Unamchelewesha pia mwekezaji kurejesha fedha alizokopa, atafilisika na kushindwa kuwekeza.” – Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

error: Content is protected !!