Siku hizi huvaaji wa pete kwenye vidole vya mikononi umekuwa kama urembo na watu wengi hufanya hivyo bila kutambua kwamba kuna maana ya jinsi mtu huvaa pete kwenye kila kidole. Mkono wa kushoto ni maalumu kabisa kwa uvaaji wa pete na wakulia wengi huvaa kama urembo.
Zifuatazo ni maana ya uvaaji pete katika kila kidole,
Kidole gumba
Pete ikivaliwa kidole gumba ni ishara ya kuwa na afya njema pamoja na mali.
Kidole cha pili
Mtu akivaa pete kidole cha pili baada ya kidole gumba basi ni ishara ya uongozi na cheo katika jamii.
Kidole cha kati
Endapo utamuona mtu amevaa pete kidole cha kati basi maana yake ni kwamba mtu huyo ni jasiri lakini pia bado yupo katika harakati zakutafuta mwenza.
Kidole cha pete
Mtu akivaa pete kwenye kidole hiki anaamaanisha kwamba tayari amekwisha oa au kuolewa.
Kidole cha mwisho
Mtu avaapo pete kidole kidogo cha mwisho basi ni ishara kwamba mtu huyu ni muaminifu, mwenye akili na mpenda familia.