Neema kwa watakao hama Ngorongoro kwa hiari

HomeKitaifa

Neema kwa watakao hama Ngorongoro kwa hiari

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali ipo tayari kulipa gharama zote kwa walio tayari kuhama kwa hiari eneo la Ngorongoro na kusisitiza wanaotaka kuondoka wasizuiliwe.

“Nasisitiza wananchi wanaotaka kuhama kwa hiari wasizuiwe na watu wengine wenye lengo la kukwamisha jitihada njema zinazochukuliwa na serikali katika kulinda urithi huu wa dunia na uhifadhi wa maeneo hayo,” alisema Majaliwa.

Majaliwa alisema hatua za awali zilizochukuliwa ni kuwafahamisha wananchi kuwa serikali ipo tayari kulipa gharama zote kwa wote walio tayari kuhama kwa hiari na zoezi hilo litazingatia haki zote za binadamu.

Aidha, aliwataka wananchi Ngorongoro walio tayari kuhamia maeneo mengine wakajiandikishe kwa Mkuuwa Wilaya ya Ngorongoro, Karatu, Mhifadhi Mkuu na Mkuu wa Mkoa na wapewe ushiriakiano unahohitajika.

 

error: Content is protected !!