Spika atoa onyo kwa mawaziri

HomeKitaifa

Spika atoa onyo kwa mawaziri

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, ametoa onyo kwa mawazari pamoja na manaibu wao kuhakikisha wanahudhuria vikao vya Bunge kutokana na baadhi yao kusuasua kushiriki vikao hivyo.

“Kuna wale ambao hawapo kwenye kikao, hajaitwa na Rais, Makamu wa Rais , wala Waziri Mkuu, wale ambao wanakuwa huko kote hawapo , wahakikishe wanakuwepo bungeni kwa sababu pamoja na kwamba wanapelekewa taarifa na utaratibu upo mzuri kabisa, ila lengo la serikali kuwa sehemu ya Bunge ni pamoja na wao kuwapo bungeni wakati hoja za wabunge zikizungumzwa na wananchi ni vizuri mawaziri wakisikiliza,” alisema Spika Tulia.

Aidha , alikemea vitendo hivyo na kusema waige mfano wa Waziri Mkuu ambaye amekuwa akihudhuria vikao vya bunge mara kwa mara na kukaa bungeni akisikiliza hoja za wabunge.

 

error: Content is protected !!