Fahamu chanzo cha ndoa ya Ali Kiba kufika mahakamani

HomeBurudani

Fahamu chanzo cha ndoa ya Ali Kiba kufika mahakamani

Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania na mmiliki wa lebo ya King’s Music, AliKiba amefunguliwa kesi na mke wake raia wa Kenya, Amina Khalef kwa tuhuma za kutotengenezewa mazingira salama na yenye utulivu katika ndoa yao pindi wapo jijini Dar es Salaam.

Amina alieleza chanzo kingine cha kufikia hatua hiyo ni tabia ya Kiba kuwa wanawake wengine, matusi na kukatishwa tamaa na wakwe zake ikiwa ni miezi 6 tu baada ya wawili hao kufunga ndoa tarehe 19 mwezi Aprili mwaka 2018 jijini Mombasa.

Alisema tena kuwa, baada ya kujifungua mtoto wao wa kwanza Februari 19,2019, Kiba alimuacha bila chakula wala mahitaji ya msingi nyumbani kwao wakati alikua ananyonyesha licha ya jitihada kufikia na kutatua masuala yao Ali hakuwa tayari katika hilo.

Katika shtaka alilofunguliwa Ali Kiba kwenye Mahakama ya Kadhi jijini Mombasa, Amina anadai talaka huku akisema ndoa hiyo haiwezi kuendelea tena, kupewa fedha za matumizi kwa ajili ya watoto kiasi cha shilingi milioni nne kwa mwezi na pia kuhudumia matibabu ya watoto wote wawili.

Aidha, mahakama imesema kwamba Ali Kiba alipewa siku 15 za kufika kwa ajili ya kesi hiyo na endapo atashindwa kufanya hivyo basi taratibu zingine zitaendelea hata bila yeye kuwepo. 

error: Content is protected !!