Abebewa mimba

HomeBurudani

Abebewa mimba

Mwigizaji nyota wa filamu za Nollywood nchini Nigeria, Ini Edo amefunguka kwa mara ya kwanza yeye ni mzazi wa mtoto mmoja na alipata mtoto huyo kupitia kubebewa mimba na mwanamke mwingine, kisayansi njia hiyo inaitwa “Surrogacy”.

Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha Lilian’s Couch huko Nigeria kinacho ongozwa na mtangazaji Lilian Afegbai, Ini amesema kwamba aliamua kutumia njia hiyo ili kupata amani ya moyo wake kwani yeye ni mtu ambaye anapenda kukaa peke yake lakini aligundua kwamba kila akiamka asubuhi hajifikirii bali anafikiria mtu mwingine.

Pia amebainisha kwamba alikosolewa na wengi kwa kuamua kupata mtoto kwa njia ya kubebewa mimba ila amewaambia mashabiki kuwa yeye ndiye alitoa yai ambalo lilitumika kuunda mimba ya binti yake na hivyo wanafanana na ni mtoto wake.

“Niliamua kufuata njia hiyo (Surrogacy) ili na mimi nitimize amani ya moyo wangu pamoja na ndoto ya kuwa na familia” alisema Ini Edo na kuongeza kwamba bado kuna mayai yake ambayo yamehifadhiwa ili kutumika ikiwa ataamua kubeba mimba mwenyewe au kubebewa na mtu mwingine.

Kuhusu baba wa binti yake huyo, Ini alisema kwamba alitafuta mbegu za mtu aliyejitolea kumpa ili asipate shida yoyote kimawazo siku za usoni. “Huwa ninashtuka kila mara nikiona mama na baba wakizozana hadharani kuhusu mtoto na ndiyo sababu nilitafuta mbegu tu.” alieleza Ini Edo. 

error: Content is protected !!