Ajali mbaya yaua watatu

HomeKitaifa

Ajali mbaya yaua watatu

WATU watatu wamefariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Mohamed Classic iliyotokea Hanang mkoani Manyara.

Basi hilo lenye namba za usajili T643 DJP lililokuwa likielekea Kigoma kutokea Arusha liligongana na Fuso  lenye namba T380DWF lililokuwa likitokea Singida kwenda Moshi, Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Waliofariki kwenye ajali hiyo ni dereva na fuso na msaidizi wake, pamoja na dereva msaidizi wa basi.

error: Content is protected !!