Akiri kuua baba na mama yake mdogo akiwatuhumu kwa uchawi Njombe

HomeKitaifa

Akiri kuua baba na mama yake mdogo akiwatuhumu kwa uchawi Njombe

Jeshi la Polisi mkoani Njombe linamshikilia Jacktani Mgeni (31) kwa tuhuma za mauaji ya Alfred Mgeni (65) na mke wake Betes Msigara (55) wote wakazi wa Ivigo wilaya ya Wanging’ombe.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo kutokana na kuwatuhumu baba yake mdogo na mama yake mdogo (marehemu) kuwa ni wachawi wanamroga mama yake aitwaye Yusta Yohana ambaye aliteguka mguu tangu Julai, 2026 na hajapona licha ya kumpeleka hospitali ya Ikonda na Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Polisi wamesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

error: Content is protected !!