Rais Samia: Wananchi tunzeni miradi inayotekelezwa na serikali

HomeKitaifa

Rais Samia: Wananchi tunzeni miradi inayotekelezwa na serikali

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Kizimkazi na maeneo mengine kutunza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali, akisisitiza kuwa miradi hiyo ni msingi wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Akizungumza Agosti 13, 2026 visiwani Zanzibar, mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji Kizimkazi, Rais Samia amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali unapaswa kulindwa ili uweze kuwasaidia wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

“Ni wajibu na ni lazima tutunze miradi hii kama tunavyotunza macho yetu. Miradi hii ni fursa zetu, ni uchumi na ustawi wa maisha yetu,” amesema Rais Samia.

Amesema miradi hiyo imeletwa kutokana na kuwepo kwa amani nchini, hivyo ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza amani ya nchi ili Tanzania iweze kupata maendeleo zaidi.

error: Content is protected !!