Aliyefumiliwa nyuzi na daktari aeleza mkasa mzima

HomeKitaifa

Aliyefumiliwa nyuzi na daktari aeleza mkasa mzima


Zubeda Ngereza, mkazi wa Kijiji cha Kerenge tarafa ya Magoma wilayani Korogwe mkoani Tanga ameeleza jinsi tabibu Jackson Meli alivyomfumua nyuzi aliyomshona kwenye jeraha baada ya kushindwa kumlipa shilingi 10,000.

Tukio hilo lilitokea Julai 28 ambapo Zubeda alipata ajali ya pikipiki na kuumia maeneo ya usoni, begani na kwenye kiwiko cha mkono wa kushoto. Alipofika Zahanati ya Kerege alipewa huduma ya kufungwa vidonda vyote katika majeraha yake.

Baada ya kupata matibabu muuguzi alidai fedha akisema kuwa gharama za kufungwa vidonda vyote kwa Zubeda pekee, ilikuwa ni 10,000, lakini Zubeda alimjibu kwamba hakuwa na fedha, hivyo asubiri kwanza awasiliane na watoto wake.

Baada kutamka hivyo tabibu alibadilika sana na kumwambia asimtanie kwani anao uwezo wa kutoa dawa zote kwenye mwili wa Zubeda alizomuhudumia, lakini alidhani ni utania, na asingeweza kufanya hivyo. Ghafla malumbano yakazidi na punde Meli alianza kutoa pamba kwenye vidonda vya Zubeda ilhali vidonda vikiwa vibichi kabisa.

Tabibu aliendelea kufanya hivyo hadi kufikia kidonda kilichoshonwa na kuanza kutoa nyuzi, licha za Zubeda kulalamika maumivu makali, huku akimwambia Zubeda aende akashitaki popote.

Wasamaria walitokea kutoa utetezi kwa Zubeda ndipo akapewa tena huduma huku Daktari Meli akishikiliwa na polisi kuanzia siku hiyo hadi Julai 30 alipoachiwa kwa dhamana.

Septemba 4, 2021 TAMISEMI ilimsimamisha kazi, na Septemba 8, 2021 Baraza la Madaktari Tanganyika lilimwandikia notisi ya siku 14 ajieleze kwa maandishi.

error: Content is protected !!