Taarifa ya serikali kuhusu ajira 10,000 za walimu

HomeKitaifa

Taarifa ya serikali kuhusu ajira 10,000 za walimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amesema wizara hiyo inasubiria kupata kibali cha kuajiri walimu 10,000 kabla ya Desemba mwaka huu.

Akizindua tawi jipya la Tume ya Utumishi wa Walimu jijini Dodoma hapo jana, Waziri Ummy amesema “Tume inatakiwa kujiandaa kuajiri mwaka huu kwani TAMISEMI inategemea kupokea kibali cha kuajiri walimu 10,000 kabla ya Desemba mwaka huu”

Ummy Mwalimu alisema hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kuhusika na kuajiri walimu badala ya wizara hivyo ameiagiza tume hiyo kukusanya takwimu katika halmashauri 139 na kupeleka orodha ya mahitaji ya walimu na upungufu uliopo hadi kufikia Septemba 21 mwaka huu.

error: Content is protected !!