Mzazi amuuza mtoto wake kwa shilingi laki moja

HomeKitaifa

Mzazi amuuza mtoto wake kwa shilingi laki moja

Septemba 7 mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya lilitangaza kuwashikilia watu wawili kwa tuhuma ya kufanya biashara ya watoto. Watu hao, Daniel Julius (21) mkazi wa Nsonga na Kamungu Julius (30) mkazi wa Rwimba walikamatwa katika Kijiji cha Mahango Wilayani Mbarali baada ya kuwauza watoto 11 kwa wafugaji ili wafanye kazi ya kuchunga mifugo.

Ilielezwa kwamba watoto hao waliokuwa na umri kati ya miaka 10 na 14,  walikuwa wanauzwa kwa gharama ya shilingi 25,000 na 30,000.

Mapya yamezuka baada ya baadhi ya wazazi wa watoto hao kujitokeza na kusema kwamba waliridhia watoto wao wauzwe. Mzazi mmoja aliyefahamika kwa jina la Kaputila Mwakalobo, mkazi wa kata ya Swaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya alisema yeye aliridhia kumuuza mtoto wake.

Alisema alifikia uamuzi kwa sababu mtoto wake alikuwa mdokozi hivyo alikuwa akimsababishia hasara. Kaputila anasema alikubaliana na wateja wake kwamba wawe wanamlipa shilingi 100,000 tu kwa mwaka kisha wamchukue mtoto wake akafanye kazi za kuchunga mifugo.

 

error: Content is protected !!