Aliyekuwa Meya wa Moshi ang’oa misaada yake

HomeKitaifa

Aliyekuwa Meya wa Moshi ang’oa misaada yake

Juma Raibu aliyekuwa Meya Mstahiki wa Manispaa ya Moshi ambaye hivi karibuni aling’olewa wadhifa huo ameamua kwenda kung’oa misaada aliyowahi kuitoa kama ikiwemo miundombinu ya maji aliyotoa siku za nyuma kwa vijana wanaofanya mazoezi na mechi.

Kwa mujibu wa mkazi wa kata ya Pasua, Waziri Shemanguzo, Raibu alifika uwanjani hapo na kung’oa mita ya maji na kuondoa nayo.

“Wakati anatoa msaada huo, Raibu aliita vyombo vya habari na kutangaza kutoa msaada kwa vijana lakini cha kushangaza safari hii amekuja kimya kimya na kung’oa bila kuwatangazia wala kutoa sababu za kung’oa,” alisema Waziri.

Alipotafutwa kuzungumzia kitendo cha kung’oa miundombinu ya maji, Raibu alisema bomba hilo lilikosa usimamizi na kusababisha bili kuwa kubwa.

“Ni kweli nilitoa msaada huo wa kuwavutia maji kwenye uwanja wa mpira Mandela, lakini maji hayo yalikuwa yakiachwa tu na kumwagika muda wote, maana palikosa usimamizi hivyo ikawa inaletwa bili kubwa,” alisema Raibu.

 

error: Content is protected !!