Filamu ya Royal Tour jijini New York leo

HomeKimataifa

Filamu ya Royal Tour jijini New York leo

Filamu ya Royal Tour inayozinduliwa leo jijini New York, nchini Marekani ambayo mhusika mkuu ni Rais Samia Suluhu Hassan, inakwenda kuitangaza Tanzania na kufungua milango ya utalii na uwekezaji nchini.

Royal Tour inazinduliwa New York kutokana na Marekani kuwa sol la kimkakati la utalii na fursa ya kuwa na wakazi wengi wanaopenda kusafiri, lakini pia ina idadi kubwa ya watu wanaojishughulisha na biashara ya utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana amesema uzinduzi wa filamu unaifanya Tanzania kujitangaza si tu kiutalii lakini pia katika nyanja nyingine za biashara, viwanda na uwekezaji.

“Sasa milango ya utalii na maeneo mengine ya uwekezaji. Tunamshukuru Rais Samia kwa maono haya, kimsingi yamekuja kwa wakati muafaka, maana hili ni jukumu letu sote,” alisema Dk. Chana.

Baada ya uzinduzi wa New York leo na Los Angeles, ratiba inaonesha kwa hapa nchini itaoneshwa Dar es Salaam Aprili 28 na Zanzibar Mei 7, mwaka huu.

error: Content is protected !!