Aliyeteuliwa atenguliwa kabla ya uapisho

HomeKitaifa

Aliyeteuliwa atenguliwa kabla ya uapisho

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali Suleiman Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na ametengua uteuzi wa Dk Raphael Chegeni.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.

Julai 28 mwaka huu Rais Samia alimteua Dk Chegeni awe Mkuu wa Mkoa wa Mara akiwa ni miongoni mwa wateule tisa wapaya kwenye nafasi hiyo.

Viongozi hao wanatarajiwa kuapishwa leo.

error: Content is protected !!