Antonio Nugaz afunguka baada ya kuondoka Yanga

HomeMichezo

Antonio Nugaz afunguka baada ya kuondoka Yanga

Kupitia instagram, Nuga amewashukuru ‘Wananchi’ huku pia akitoa ahadi ya ‘kuonana nao tena’, japo haijafamika ataonana nao kwa namna gani.

Nugaz ameandika

“Kwa udhati wa Moyo wangu naomba niwashukuru Kuanzia Uongozi wote wa Yanga chini ya mwenyekiti wetu Dk. Mshindo Mbette Msolla na Kaimu Katibu Mkuu Mpya Senzo Mbatha Mazingiza, wafanyakazi wenzangu wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka miwili niliyoitumikia @yangasc kwa moyo Mkunjufu na kujitoa kwangu, Mungu awabarik, awalinde na awape kila hitajio la nafsi zenu ili tuweze kuipeleka mbele Brand ya Yanga.Wanachama,wapenzi na mashabiki wa Yanga ninyi mumekuwa na mimi kwa moyo mmoja Ahsanteni sana Nawapenda sana na nitaendelea kuwa nanyi.Tutaonana tena hivi Karibuni. Insha Allah.”

Yanga imetangaza kuachana na Nugaz ambaye alikuwa Afisa Mhamasishaji wa timu hiyo kwa miaka miwili baada mkataba wake kumalizika

error: Content is protected !!