Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetangaza kuanza safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) hatua inayolenga kupanua mtandao wake wa safari barani Afrika.
Safari hizo zitafanyika mara nne kwa wiki, kila siku ya Jumapili, Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na zitachukua chini ya saa nne kufika kinshasa.
Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Uhusiano wa Mawasiliano wa ATCL, Sarah Reuben, aliyebainisha kuwa kuanza kwa safari hizo, ATCL itatoa zawadi ya punguzo hadi Dola 50 za Kimarekani.