Televisheni ya mtandaoni ya Millard Ayo (AYO TV) inatakiwa kuomba radhi siku tatu mfululizo baada ya kuchapisha maudhui yanayoonyesha miili ya watoto wa shule ya Msingi ya King David, waliofariki dunia katika ajali ya gari mkoani Mtwara hivi karibuni.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kujiridhisha kwamba utetezi uliotolewa na Ayo TV ni hafifu na hivyo televisheni hiyo imekiuka kanuni ya mawasiliano ya kieletroniki na posta ya maudhui mtandaoni ya mwaka 2022.
Aidha, TCRA imeagizi kituo hicho kuhakikisha kinazingatia utu, kanuni, msingi sheria na viwango katika uchapishaji na uandaaji wa wa habari zake.